Kocha mpya anakunja Sh9 milioni kwa siku

KOCHA mpya wa Mabingwa wa Misri, Al Ahly ambaye ni raia wa Afrika Kusini, Pitso Mosimane atalipwa mshahara wa Sh 9.8 milioni kwa kila siku ya Mungu.

 

Hiyo inamaanisha kwamba kwa wiki atakuwa anakunja Sh 69 milioni. Twende sawa, unajua kwa mwezi atakuwa analipwa Shilingi ngapi?  Sh 277 milioni.

 

Kocha huyo amejiunga na klabu hiyo iliyopania kubeba ubingwa wa Afrika msimu huu akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo ilikuwa ikimlipa Sh 139 Milioni kwa mwezi.

 

Mbali na fungu hilo la mshahara, kama atatwaa ubingwa wa Misri au ule wa Ligi ya Mabingwa Afrika atalipwa Sh.1.1Bilioni.

 

Timu yoyote ile ambayo itataka kusitisha mkataba wake na Ahly italazimika kulipa mshahara wa miezi sita ambao ni zaidi ya Sh.1.6 Bilioni.

 

Simba hivi karibuni ilitembelea makao makuu ya Ahly kutaka kujifunza mambo mbalimbali juu ya maendeleo ya klabu hiyo.