Kocha Yanga apangua kikosi

Sunday September 13 2020

 

KOCHA mkuu wa Yanga Zlatko Krimpotic, amefanya baadhi ya mabadiliko kwenye kikosi chake katika mechi yao inayotarajia kuanza saa 1:00 usiku, mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam dhidi ya Mbeya City.
Katika kikosi chake, Zlatko amewaondoa nyota wake wanne walioanza kikosi cha kwanza mchezo uliopita dhidi ya Prisons ambapo walitoka sare ya bao 1-1 huku mmoja pekee Nchimbi akianzia benchi wakati nyota watano wakiingia kikosi cha kwanza.
Kikosi cha leo Jumapili, Septemba 13, 2020, golini amemuweka Metacha Mnata wakati mechi iliyopita alisimama Farouk Shikalo, Lamine Moro amechukuwa nafasi ya Abdallah Shaibu 'Ninja'. Shikalo na Ninja leo hawapo hata kwenye wachezaji wa akiba.

Tunombe Mukoko yeye ameanza akichukuwa nafasi ya Mauya ambaye ameanzia benchi, Haruna Niyonzima ameanza akichukuwa nafasi ya Ditram Nchimbi ambaye yupo benchi huku Tuisila Kisinda mechi iliyopita alianzia benchi leo ameanza akichukuwa nafasi ya Farid Musa ambaye hayupo kabisa kikosini.
KIKOSI CHA LEO vs MBEYA CITY
Metacha Mnata, Mbwana Shomari, Yassin Mustapha,  Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Tonombe Mukoko, Deus Kaseke, Fei Toto, Michael Sarpong, Haruna Niyonzima na Tuisila Kisinda.
Wachezaji wa akiba ni Ramadhan Kabwili, Adeyun Saleh, Said Juma, Zawadi Mauya, Carlinhos, Songne Yacouba na Ditram Nchimbi.
KIKOSI KILICHOPITA vs PRISONS
Shikalo, Shomari, Yassin, Ninja, Mwamnyeto, Mauya, Kaseke, Sarpong, Nchimbi na Farid Musa.
Wachezaji wa akiba walikuwa ni Mnata, Lamine, Niyonzima, Carlinhos, Mukoko, Kisinda na Yacouba.


Advertisement