Kocha Mbao awapa neno TFF

Muktasari:

Mbao ni moja ya timu inayopambana kujinasua na janga la kushuka daraja kwani iko nafasi ya pili kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23.

KOCHA wa Mbao Fc, Abdulmutic Haji amefurahi kusikia Ligi Kuu inarejea wakati wowote lakini amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwapima kwanza wachezaji wa timu zote kabla ya kuruhusu ligi kuanza.

Ligi Kuu Bara pamoja na michezo mingine ilisimama kwa miezi miwili sasa kutokana na mlipuko wa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona.

Hata hivyo leo  Alhamisi katika hafla ya kuwaapisha viongozi iliyofanyika katika Ikulu ya Dodoma, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli  ametangaza rasmi kuruhusu michezo kuendelea kuanzia Juni Mosi.

"Nimesikia Ligi inaweza kuanza muda wowote lakini tunasubiri tamko rasmi kutoka TFF ambao ndio wanaopanga tarehe rasmi ya kuanza ligi ndipo tuanze kuwapa taarifa wachezaji za kuwaita mazoezini.

" Pia TFF wanatakiwa kwanza kuendesha zoezi la upimaji wa ugonjwa huo kwa wachezaji wa timu zote kabla ya kuruhusu time kuanza mazoezi na hata ligi kwa sababu ukiangalia kila mmoja ametoka sehemu tofauti tofauti hivyo huwezi kujua kama tayari ana maamumbizi au la, waige mfano Kama wenzetu anavyofana mfano kwenye ligi ya Uingereza.

"Ingekuwa ni marelia ni rahisi kwani sehemu yoyote tungeweza kuwapima wenyewe wachezaji lakini corona ina kipimo chake maalum hivyo TFF wanatakiwa kusimamia hilo ili ligi ikirejea wote tuwe salama" amesema Haji.

Pia Haji ameitaka TFF kutoa muda wa angalau wiki mbili ili timu ziweze kujiandaa kabla ya kuendelea na ligi.

" Lazima tupate angalau siku 10 au zaidi ili kuwaweka wachezaji wetu sawa kwa sababu kila mmoja alikuwa anafanya mazoezi binafsi hivyo sasa huwezi jua wako fiti kwa kiwango gani ndio maana lazima wawe pamoja kwa muda ili ike ari ya timu irejee" amesema Haji.