Klopp ahofia jambo kwa kinda wake

Thursday October 29 2020
klopp pic

LIVERPOOL, ENGLAND. KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema ana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha anamjenga kisaikolojia beki wake, Rhys Williams ili aendelee kuonesha kiwango kikubwa kwani watu wengi watakuwa wanamzungumzia baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Midtjylland Jumanne iliyopita.

Williams aliingia dakika ya 30 katika mchezo huo ambao Liverpool ilishinda mabao 2-0, akichukua nafasi ya Fabinho aliyepata majeraha ambayo huenda yakamuweka nje muda mrefu.

“Amecheza kwa kiwango kikubwa. Ubaya ni kwamba tuna siku nne za kujiandaa kabla ya kukutana na West Ham, nafahamu stori kubwa itakuwa ni yeye kutokana na kiwango alichoonyesha na shida itakuwa anavyopokea sifa hizo.

Upande wetu tunajaribu kupambana kuhakikisha tunamfanya anatuliza mihemko ili aje kuonesha kiwango kikubwa,”alisema Klopp

Mchezaji huyo ni zao la Akademi ya Liverpool na msimu uliopita alikuwa anacheza kwa mkopo huko Kidderminster inayoshiriki madaraja ya chini hapo England na kuonyesha kiwango mikubwa jambo ambalo linamfurahisha Klopp.

 

Advertisement
Advertisement