Klopp, Lampard watia neno kuchezwa wa waamuzi wanawake

Wednesday August 14 2019

 

By Eliya Solomon

London, England.Kocha wa Liverpool, Jürgen Klopp ametania kuwa hutoonyesha ukali kwa mwamuzi wa kike Stephanie Frappart atakayechesha mechi ya leo UEFA Super Cup kati ya Liverpool na Chelsea.

Mwanamama Stephanie raia wa Ufaransa, ataweka rekodi kwa kuwa mwamuzi wa kwanza wa mwanamke kucheza mchezo huo mkubwa wa UEFA huku akisaidiwa na wanawake wenzake Manuela Nicolosi na Michelle O'Neill.

"Nitajaribu kutokuwa mkali ili nisiufanye mchezo kuwa mgumu kwao. Nitaonyesha sura ya upole na upendo  vinginevyo mama atachukizwa nami nyumbani," anatania jamani.

Klopp ambaye aliipa Liverpool taji la sita la Ligi ya Mabingwa Ulaya, alisema anajisikia kuwa mwenye furaha kuwa sehemu ya tukio la Kihistoria ambalo litafanyika leo, Uturuki.

Alisema hatimaye muda umefika wa historia kuweka, itakuwa mara ya kwanza kwa mwanamke kuchezesha mchezo mkubwa kama huo, lakini akadai haitakuwa mwisho kwa waamuzi wa kike kuaminiwa.

"Uamuzi yaliyofanywa ni makini na naamini wako vizuri ndio maana wamepewa huu mchezo," alisema kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund.

Advertisement

Frappart ambaye Aprili alikuwa mwamuzi pekee kuchezesha Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’ alisema kuna ugumu kucheza mechi ya wanaume huchangiwa na ushindani uliopo baina yao.

Kocha wa Chelsea, Frank Lampard alisema mchezo huo, utakuwa na mvuto wa aina yake kutokana na kuchezeshwa na wanawake kwa mara ya kwanza.

"Najua duniani kote wanawake watafuatilia wapenda michezo kuona vile ambavyo wenzao wanaenda kuweka histotia," alisema kocha huyo ambaye timu yake ilianza vibaya msimu huu wa Ligi Kuu England.

Advertisement