Kiungo Misri atimuliwa kambini kwa kashfa

Wednesday June 26 2019

 

Cairo, Misri. Kiungo wa Misri, Amri Warda ametimuliwa leo kambini taarifa ya Shirikisho imesema.

Taarifa iliyotoka mchana huu ni kwamba baada ya vikao kadhaa juu ya sakata la utovu wa nidhamu kiungo huyo ameamuriwa kuondolewa kambini.

Ingawa taarifa hiyo haikuanisha ni aina gani ya utovu wa nidhamu, lakini imefahamika kwamba kosa la kiungo hiyo ni kuvuja kwa video yake akifanya kitendo cha uchafu.

Warda ambaye ni kiungo wa klabu ya PAOK ya Ugiriki sasa anakuwa mchezaji wa tatu kuondolewa kambini akitanguliwa na kiungo mwingine wa Algeria, Haris Belkebla.

Belkebla aliondolewa mapema kabla ya Algeria kutua Misri kutokana na kuvuja kwa video yake ya uchaguzi hatua ambayo ilimkera kocha Djamel Belmadi na kuamua kumtimua.

Mwingine ni mshambuliaji wa Burundi, Seleman Ndikumana ambaye aliondolewa haraka kambini wakati tayari akiwa ndani ya ardhi ya Misri.

Advertisement

Advertisement