Kitenge amvulia kofia Kichuya

Muktasari:

Kama kuna kitu amekiona straika wa Stand United 'Chama la Wana' Alex Kitenge kwa winga wa Simba, Shiza Kichuya ni namna anavyotumia mwili wake mdogo mbele ya mabeki.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Stand United 'Chama la Wana', Alex Kitenge amevutiwa na kiwango kizuri cha kiungo wa Simba, Shiza Kichuya baada ya mechi yao ya jana Jumapili.

Kitenge amebaini Kichuya ni mchezaji mwenye pumzi, kasi na anatumia akili nyingi kulazimisha mashambulizi.

"Nilikuwa natamani kuwaona Kichuya, Meddie Kagere kama ana kasi ile ile ambayo alikuwa nayo akiwa Gor Mahia bado yupo fiti, lakini pia  John Bocco ambaye hajacheza, nimejifunza mengi kwao.

"Mfano Kichuya ana mwili mdogo mdogo sana, lakini ana akili ya kutowafuata mabeki anakuwa anawapiga chenga, akiendelea hivyo na kuongeza juhudi zaidi atafika mbali na awe mawazo ya kutoka nje ya nchi yake Tanzania," alisema Kitenge.

Katika mchezo huo Stand United ilikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba kwenye Uwanja wa Taifa.