Kisura Mwanza ndiye malkia wa Kanda ya Ziwa

Saturday August 3 2019

 

By Saddam Sadick,Mwanza

SYLVIA Sylvester kutoka Mwanza ameibuka mshindi katika shindano la kumsaka Mrembo wa Kanda ya Ziwa, 'Miss Lake Zone 2019' baada ya kuwabwaga wapinzani wake 19 aliokuwa akichuana nao.
Katika mchuano huo ambao umefanyika usiku huu kuamkia leo katika ukumbi wa Bunder Sliga Sports Bar iliyopo Nyasaka jijini hapa,kila mshiriki alitumia mbinu kuweza kuwashawishi majaji na Mrembo huyo kuweza kupita.
Kwa ushindi huo Sylvester amejipatia Sh 1.2 milioni,wa pili Suzan Faustine aliyepokea Sh 700,000 na wa tatu Rebecca Manoti kutokaSimiyu aliyezawadiwa Sh 500,000.
Pia Jesca Nzigo (Mwanza) ambaye aliishika nafasi ya nne alichaguliwa kuwa balozi wa Bunder Sliga Sports Bar na kuzawadiwa kitita cha Sh 200,000 kutoka kwa Meneja Regina Magasha.
Jumla ya washiriki 20 kutoka mikoa mitano ya Ukanda huo ikiwa ni wanza, Simiyu, Shinyanga, Mara na Kagera walishiriki shindano hilo.

Advertisement