Kissu amtega Ndayiragije Stars

KIPA David Kissu wa Azam Fc ameanza Ligi Kuu akiwa na msimu mzuri na ni kama amemtega Kocha wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije kwenye kikosi kitakachotajwa Oktoba 2 kuikabili Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopo kwenye kalenda ya Fifa.

Kissu awali alikuwa akiitwa Stars akiwa Gor Mahia ya Kenya lakini hakupata nafasi ya mbele ya Aishi Manula (Simba SC), huku Gor Mahia alikuwa akipata nafasi ya kuanza.

Akizungumza na Mwanaspoti,” Kissu alisema.

“Siwezi kuizungumzia nafasi yangu moja kwa moja timu ya Taifa kwa maana mchaguzi ni kocha kuona kama naweza kumsaidia, kwangu mimi ni kuonyesha nilicho nacho na kocha akiridhia atanipa nafasi.”

Akizungumzia kujitoa kwa wachezaji wenzake Azam, anasema ni kutokana na kila mmoja kutaka kufanya vizuri msimu huu.

“Tunataka kuchukua ubingwa na kila mchezaji anataka kutimiza ndoto hiyo, ndio maana hata kutoruhusu goli sio mimi tu peke yangu bali huanzia kule mbele mpaka kwenye safu ya ulinzi,” alisema.

Kisu katika mechi nne alizocheza hajaruhusu bao ikiwa ni tangu asajiliwe na Azam FC baada ya kumaliza mkataba wake na Gor Mahia aliyokuwa anacheza msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Kenya.