Kisinda: Uwanja uliniudhi

Muktasari:

Uwanja wa Jamhuri umefungiwa kutumika mechi za Ligi kutokana na ubora mdogo wa eneo la kuchezea, maeneo ya kukalia wachezaji wakati wa mechi na vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji.

Winga wa Yanga, Tuisila Kisinda amesema hana shida katika kucheza kwenye viwanja vya ubora wa kawaida lakini ule wa Jamhuri ni kiboko.

Akizungmza mara baada ya mchezo huo Kisinda amesema uwanja huo hauna hadhi ya kuchezewa mechi za Ligi kutokana na ubovu wa sehemu ya kuchezea.

Winga huyo Mkongomani amesema hali ya uwanja huo unamlazimu mchezaji kutumia muda mrefu kumiliki mpira na kumnyima uhuru wa kufanya anachotaka kukifanya.

"Mpira hautulii kila ukitaka kujipanga unakuta tayari wapinzani wamefika eneo hilo, ni uwanja mbovu sana uliniudhi, amesema Kisinda.

"Sina tatizo katika kucheza kwenye viwanja vya kawaida lakini huu wa Jamhuri ulikuwa mbovu zaidi na hauna hadhi kabisa ya kuchezewa Ligi kubwa kama hii.

Aidha Kisinda akizungumzia hatua ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuufungia amesema uamuzi huo ni sahihi na kwamba anaunga mkono na kuwataka wahusika kuutengeneza.

"Wamefanya uamuzi sahihi kabisa sio uwanja mzuri wanatakiwa kuutengeneza unazifanya timu kucheza nje ya malengo yao.