Kipigo UEFA champa akili Jurgen Klopp

Muktasari:

  • Kocha huyo alisema sasa wanafanya kazi kuhakikisha mechi yao ijayo dhidi ya PSG wanafanya kazi ya ziada kushinda na pia kuhakikisha wanashinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Napoli itakayopigwa huko Anfield.

LONDON,ENGLAND.KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp anakuna kichwa na sasa anatafuta dawa ili kufuzu mechi za Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mabao mawili ya kipindi cha kwanza ya Milan Pavkov yameifanya timu hiyo iliyocheza fainali ya Ulaya msimu uliopita kufikisha mechi tatu za kupoteza nje ya England katika michuano hiyo.

Kocha huyo alisema sasa wanafanya kazi kuhakikisha mechi yao ijayo dhidi ya PSG wanafanya kazi ya ziada kushinda na pia kuhakikisha wanashinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Napoli itakayopigwa huko Anfield.

“Tutalazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye timu, ili kupata matokeo tunayoyataka,” alisema Klopp, ambaye katika mchezo wa juzi Jumanne usiku aliwaacha benchi, Roberto Firmino na Joe Gomez na kuingia kipindi cha pili.

“Mwishoni, naweza kusema kuwa mipango yangu haikufanya kazi. Tunatakiwa kuhakikisha kufungwa huku hakutokei tena na kama mechi ijayo na PSG tusipopata matokeo lazima tukaze kwa Napoli.

“Kwanza tuhakikishe Paris tunashinda. Kuna mambo lazima kuyafanya yawe makubwa ili kuwa na matokeo mazuri,” alisema.

“Hakuna namna, tunatakiwa kushinda bila kujali tunacheza wapi. Tulipanga kwa juzi usiku, lakini haikuwezekana.

“Pamoja tumefungwa, lakini haikutushangaza sana. Kama umeona mchezo wa kwanza, ilivyokuwa. Mechi ya kwanza tulitawala vizuri, lakini marudiano tulishindwa kufanya kweli kuwadhibiti,” alisema.