Kipa Serengeti kupikwa upya

Muktasari:

  • Habari ambazo Mwanaspoti ilizipata ni kwamba wachezaji wawili wa Serengeti, Tepsi Evans na Foba wameondolewa baada ya kufanyiwa vipimo vya mwisho na CAF na kluonekana kuwa vijeba.

MASHABIKI wa soka wamepagwa baada ya kushuhudia timu ao ya Vijana U17 Serengeti Boys ikipoteza mbele ya Nigeria kwa mabao 5-4, lakini ishu kubwa ni namna mechi hiyo iliyozalisha mabao mengi, lakini kumbe hata benchi kla ufundi la timu hiyo nao wameshtukia jambo na kujipanga.

Unaambiwa kabla ya mchezo wa kesho Jumatano kati ya vijana hao dhidi ya Uganda, kuna mipango imewekwa ili kumtengeneza upya kipa Mwinyi Yahya kusudi ili yasijulie yale mabao yaliyowapa ushindi Golden Eaglets, huku benchi likiri timu nzima haikucheza kama walivyotarajia.

Serengeti na Uganda zinakutana zikiwa zimetoka kupoteza mechi zao, kwani hata Uganda walilala 1-0 kwa Angola na mechi yao ni muhimu kwa hatma ya Ukanda wa Afrika Mashariki katika mbio za kwenda Fainali za Kombe la Dunia U17 zitakazofanyika baadaye mwaka huu kule Brazili.

Kocha Mkuu wa Serengeti, Oscar Mirambo alisema tangu baada ya mengi mipango yake ilikuwa ni kufumua upya nafasi ya kipa, akidasi Yahya alionyesha kiwango kizuri mechi iliyopita kwa kuokoa michomo, lakini alifanya makosa ya wazi hasa kwa mabao mawili kati ya matano waliyofungwa.

Mirambo alisema katika kikosi chake mara zote huwa wanafanya mazoezi ya kuwa na akili moja katika kuzuia pindi wanapopoteza mpira na hivyo pindi wanapokuwa na mpira wakati wanapanga au kwenda kushambulia.

“Ni kweli kuna makosa yameonekana eneo la kipa lakini tutamwelekeza upya akiwa chini ya kocha wake ili kuonesha ubora zaidi mechi ya pili ambayo tutacheza na Uganda, naamini atafanya vizuri mchezo huo kuliko huu wa kwanza,” alisema kocha huyo na kuongeza;

“Wakati wa mapumziko niliwaelekeza kwamba tunatakiwa kupambana muda wote na uwezo wa kufanya hivyo tunao, ndio maana walibadilika katika kipindi cha pili.”

Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Uganda, Mirambo alisema mchezo huo ni umuhimu mkubwa kwani ndio utakaotoa taswira ya wao kuendelea mbele.

“Tulitaka matokeo mchezo huu lakini hatukufanikiwa, hivi sasa tunaangalia michezo ya mbele yetu bado tuna michezo miwili mkononi tutajitahidi kupata matokeo,” alisema.

Naye kocha wa makipa wa timu hiyo, Peter Manyika alikiri kuna changamoto eneo hilo baada ya kipa wao kuondolewa kucheza fainali hizo.

Habari ambazo Mwanaspoti ilizipata ni kwamba wachezaji wawili wa Serengeti, Tepsi Evans na Foba wameondolewa baada ya kufanyiwa vipimo vya mwisho na CAF na kluonekana kuwa vijeba.

Wachezaji wengine walioondolewa katika vipimo vya MRI ni Camal Ryan Moumbagna, Aliou Souleymanou Hendji, Arci-En Ciel (Cameroon) na Alpha Boubacar Keita (Guinea).