Kila alipo Ronaldo, taji lipo

Muktasari:

  • Vijana wa Massimiliano Allegri walikuwa nyuma baada ya Nikola Milenkovic kupiga bao la kuongoza kwa Fiorentina kabla ya Alex Sandro kusawazisha dakika ya 37.

Turin,Italia. ACHANA na matokeo ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Ajax kwa kufungwa mabao 3-2, unaambia kila alipo Ronaldo ama magoli au kombe lazima litakuwepo.

Wakati akitoka Sporting Lisbon kwenda Manchester United 2003 kwa dau la Pauni 12.24 million, timu hiyo ilitwaa ubingwa wa England, Kombe la FA na Ngao ya Hisani.

Baada ya miaka tisa, alitua Real Madrid mwishoni mwa msimu wa 2009–10, akiweka rekodi ya dunia ya Pauni80 milion na kuiwezesha timu yake kutwaa taji la La Liga msimu wa 2011-12 na ubingwa wa Copa del Rey.

Ronaldo aliyesajiliwa Juventus akitokea Real Madrid kwa dau la Pauni99.2mil, aliipa mafanikio timu hiyo ya Bernabeu, lakini sasa si katua Juve, na mwendo ni huo huo wa vikombe.

Baada ya kujihakikishia taji la kwanza na Juventus akatangaza sasa anataka kustaafia Serie A na Juventus na furaha yake imekuwa mara mbili hasa baada ya kuifunga Fiorentina.

Vijana wa Massimiliano Allegri walikuwa nyuma baada ya Nikola Milenkovic kupiga bao la kuongoza kwa Fiorentina kabla ya Alex Sandro kusawazisha dakika ya 37.

Dakika chache baada ya mapumziko, Ronaldo alinyunyiza majalo na beki wa Fiorentina, Pezzella ikambabatiza na kujifunga.

“Nimefurahi kutwaa ubingwa wa Italia msimu wangu wa kwanza,” alisema Ronaldo.

“Of course, mambo hayakuwa mazuri Ligi ya Mabingwa, lakini msimu ujao tumo.”

Juve imetwaa ubingwa wa Italia mara ya 35 aliwahi kutua England, Manchester United ikatwaa ubingwa, alikwenda Hispania, Real Madrid ikawa hivyo na sasa yuko Italia na Juve na imetwaa ubingwa.