Kiemba atabiri mchezo wa Stars na Kenya

Saturday July 27 2019

 

By Yohana Challe

MKONGWE wa soka nchini, Amri Kiemba amesema mchezo wa kesho Jumapili baina ya Taifa Stars na Kenya 'Harambee Stars' utakuwa mgumu kutokana na ujirani wa nchi hizo.
Tanzania inasaka tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN) 2020 zitakazofaniaka mwakani nchini Cameroon.
"Klabu nyingi zilikuwa kwenye maandalizi ya ligi na michuano mbalimbali hivyo hakuna maandalizi ambayo yalifanywa kwaajili ya mchezo huu na kupata ushindi kwenye soka inatakiwa kufanya maandalizi mazuri,"
Aliongeza wachezaji wengine wakiwemo wachezaji kutoka timu ya Simba, Ibrahim Ajibu, Aishi Manula, John Bocco, Erasto Nyoni na Gadiel Michael wamejiunga na wenzao juzi jambo ambalo litampatia ugumu flani kocha wa Stars, Etienne Ndayiragije.
Jambo lingine ambalo amelitaja kama kikwazo kwa Stars ni kubadilishwa kwa kocha tena kwa muda mfupi wakitoka kwenye mashindano makubwa (Afcon) na sasa wanaingina CHAN hilo pia litakuwa mtihani.
 

Advertisement