Kichuya aukubali usajili wa Simba wa nyota kama Bocco, Kapombe na Manula

Tuesday June 20 2017

 

By Fredrick Nwaka, Mwananchi fnwaka@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amesema anaamini timu yake itafanya vizuri kutokana na usajili inaofanya.

Simba imesajili wachezaji saba hadi sasa akiwemo Ally Shomari kutoka Mtibwa Sugar, John Bocco, Shomari Kapombe na Aishi Manula waliosajiliwa kutoka Azam FC.

Akizungumza na mtandao huu Kichuya ambaye alikuwa mfungaji bora wa Simba msimu uliopita alisema wachezaji wapya wataleta changamoto kikosini.

“Ni usajili mzuri ambao utaongeza changamoto kwenye timu, naamini tutakuwa na timu nzuri msimu ujao kwa kuwa wachezaji waliosajiliwa ni wazoefu na Ligi,”alisema Kichuya aliyefunga mabao 12 katika Ligi Kuu na kuiwezesha Simba kushika nafasi ya pili na kuchukua ubingwa wa Kombe la FA.

 

Advertisement