Kichuya aikataa Simba kweupe

Muktasari:

“Acha watu waendelee kuelea hivyo, lakini ukweli ni kuwa nimesajiliwa Namungo kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wangu na Simba.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Shiza Kichuya amesema kwa sasa ni mali halali wa Namungo FC na sio kwamba, yuko kwa mkopo katika kikosi hicho. Kichuya alisema anashangazwa na taarifa zinazodai kwamba, ametua kwa mkopo kuitumikia Namungo itakayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

“Acha watu waendelee kuelea hivyo, lakini ukweli ni kuwa nimesajiliwa Namungo kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wangu na Simba.

“Ninachowaambia mashabiki wangu kuwa maisha ni yale yale hapa ni kubadilisha mazingira, nilianza Morogoro (Mtibwa Sugar) nikaenda Simba na sasa nipo Namungo,” alisema Kichuya.

Kichuya amejiunga kwa mkataba wa miaka miwili Namungo FC, alisema kikubwa ambacho atakikosa

ni sapoti ya mashabiki wa Simba walivyokuwa karibu na timu yao. Hata hivyo, Kichuya hakuweka bayana sababu za kushindwa kwake kukipiga Pharco FC ya Misri ambayo nayo ilimpeleka kwa mkopo ENPPI SC huku akisema ni mambo ambayo sio rahisi kuyaelezea na watu wakaelewa kwa undani.

Winga huyo ametua Namungo kwa pendekezo la kocha mkuu, Hitimana Thierry ambaye anaamini atawasaidia kwenye mashindano ya kimataifa. “Kichuya ni mcheza mzuri na tunaamini ataisaidia timu kutokana na uzoefu aliokuwa nao ndio sababu nikashauri asajiliwe,” alisema Hitimana.

Tayari timu Namungo imesajili wachezaji nane akiwemo, Sixtus Sabilo kutoka Polisi Tanzania, Stephen Sey (Singida United), Amani Kyata akitokea Kariobangi Sharks ya Kenya, Haruna Shamte kwa mkopo akitokea Simba. Wengine, Iddi Kipagwile kwa mkopo kutoka Azam FC, Jafar Mohamed (Yanga), Frank Magingi (Mwadui FC), Abdulhalim Humoud (Mtibwa Sugar) na Fredy Tangalo kutoka Lipuli FC.

Tayari wachezaji wote wamejiunga na kikosi hicho kwa maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba