Kelvin John ang'ara Afcon U17

Muktasari:

Goli hilo liliwaamsha vijana wa Serengeti Boys kwani walionekana kucheza kaa kushambulia zaidi na dakika 55 Edson Mshirakandi aliwachambua mabeki wa Nigeria ndani ya 18 na kudondoshwa na Muamuzi Issa Sy kutoka Senegal alionyesha kuwa penalti.

 BAADA ya kupigwa 1-3 katika kipindi cha kwanza, wachezaji wa Serengeti walionekana kuishiwa nguvu kwa kichapo hicho.

Lakini baada ya kwenda mapumziko na kurejea wachezaji hao walionekana kuanza mpira kwa spidi na kuonyesha kabisa wanahitaji magoli tofauti na kipindi cha kwanza.

Serengeti walianza kutumia mipira mirefu na dakika 55 Kelvin John 'Mbappe' alipokea pasi ndefu na kutuliza mpira akiwa mbele kidogo ya kuanzia mpira na kuoiga shuti kali ambalo lilienda moja kwa moja wavuni.

Goli hilo liliwaamsha vijana wa Serengeti Boys kwani walionekana kucheza kaa kushambulia zaidi na dakika 55 Edson Mshirakandi aliwachambua mabeki wa Nigeria ndani ya 18 na kudondoshwa na Muamuzi Issa Sy kutoka Senegal alionyesha kuwa penalti.

Nahodha Maurice Abraham aliweza kuwanyanyua mashabiki baada ya kupiga penalti hiyo iliyokuwa ya kimadaa baada ya kumgonga kipa wa Nigeria, Suleman Shaibu kwa nyuma na kutinga wavuni.

Vijana wa Nigeria walionyesha kuhitaji goli lakini safu ya ulinzi ya Serengeti inayoongozwa na Arafat Swakali ilikuwa makini kuhakikisha nyavu zao haziguswi tena.

Dakika 58 Kelvin John 'Mbappe' aliwachambua mabeki wa Nigeria na kutulia na mpira kisha kupiga pasi ya mwisho kwa Pascak Msindo aliyrpiga shuti na beki wa Nigeria aliunawa na muamzui kuweka penalti.

Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Edmund John aliwainua mashabiki baada ya kupiga penalti maridadi kwa kumuuza kipa wa Nigeria. Baada ya goli hilo liliifanya Serengeti kuwa mbele kwa magoli 4-3 huku uwanja ukiwa na shamgwe kila kona.

Nigeria hawakuonyesha kukata tamaa kwani walizidi kupeleka mashambulizi na dakika 72 aalipata goli kupitia kwa Wisdom Ubani. Spidi yao ilionekana kuzaa matunda kwani vijana wa Serengeti walikuwa wanafunguka kutaka magoli na wao kuzidi kushambulia.