Kaseja, Ajibu, Mkude warudi Taifa Stars kuivaa Kenya

Monday July 15 2019

 

By Charity James

Dar es Salaam. Kipa mkongwe Juma Kaseja, Salum Aiyee pamoja na Ibrahimu Ajibu na kiungo Jonas Mkude wameitwaa katika kikosi cha kwanza za wachezaji 25, Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa kujiandaa na mchezo wa Chan dhidi ya Kenya.

Kaseja ameitwaa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Stars baada ya kukaa nje timu hiyo kwa zaidi ya miaka mitano.

Kaseja atashindana na wadogo zake Aish Manula kipa namba moja Tanzania kwa sasa pamoja na kipa mpya wa Yanga, Metacha Mnata.

Katika kikosi hicho cha kwanza cha Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Etiene Ndayiragije kinachoonekana kujaribu kutuliza kelele za mashabiki katika uteuzi wake.

Ndayiragije amewarudisha kundini wachezaji vipenzi vya mashabiki Ibrahim Ajibu na Jonas Mkude ambao mtangulizi wake Emmanuel Amunike aliwatema na kuzua zogo kila kona ya nchini wakati wa fainali za Afcon.

Mrundi huyo amemwita kwa mara ya kwanza aliyekuwa mfungaji bora wa pili wa Ligi Kuu, Salum Aiyee wa KMC ambaye msimu uliopita alifunga mabao 18 katika Ligi Kuu Bara akiwa na Mwadui.

Advertisement

Mrundi huyo amewajumuisha kiungo mpya wa Yanga, Abdulaziz Makame pamoja na beki chipukizi Paul Godfrey.

Pia, chipukizi Kelvin John ameitwaa katika kikosi hicho cha wachezaji 25, huku kiungo wa Azam fc, Salum Abdubakar ‘Sure Boys’ na Hassan Dilunga wa Simba

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kikosi hicho kitacheza mechi ya kwanza Julai 28, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na marudiano yanatarajia kuwa Agosti 4 mwaka huu nchini Kenya.

Mshindi wa mchezo kati ya Tanzania na Kenya atacheza na mshindi wa mechi kati ya Burundi na Sudan Kusini kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika Cameroon kati ya Januari na Februari 2020.

Kikosi cha Tanzania.

Makipa: Juma Kaseja (KMC), Aishi Manura (Simba), Metacha Mnata (Yanga).

Mabeki: Paul Godfrey (Yanga), Boniface Maganga (KMC), Gadiel Michael (Simba), Paul Ngalema (Namungo), David Mwandika (Azam), Idd Mobi (Polisi Tanzania), Kelvin Yondani (Yanga), Erasto Nyoni (Simba).

Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdulazizi Makame (Yanga), Mudathil Yahya (Azam), Ibrahim Ajibu (Simba), Salum Aboubakari (Azam), Feisal Salum (Yanga), Frank Domayo (Azam), Hassan Dilunga (Simba).

Washambuliaji: John Bocco (Simba), Salum Aiyee (KMC), Iddy Nado (Azam), Ayuob Lyanga (Coastal Union), Kelvin John (U-17) na Shabani Chilunda (Azam).

Advertisement