Kapombe safi, apewa program maalum Sauzi

Muktasari:

Kapombe alikuwa nje ya uwanja kwa nusu msimu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu

Rostanburg. Beki wa Simba, Shomari Kapombe amepewa programu maalumu ya matibabu na masharti ili atakaporudi uwanjani acheze kwa kiwango bora.

Shomari alikuwa nje ya uwanja muda mrefu akiuguza jeraha la kifundo cha mguu aliyoumia akiwa kambini na timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’.

Kapombe ni beki tegemeo katika nafasi ya beki ya kulia licha ya mara kadhaa kumtumia kiraka Erasto Nyoni.

"Niligundua tatizo moja kwa Kapombe eneo la kifundo cha mguu katika viungo. Tunaendelea na matibabu apone," alisema mtaalamu wa viungo Mjerumani Paul Gomez.

Mtaalamu huyo alisema amempa masharti Kapombe namna bora ya kucheza uwanjani ili kuepuka majeraha.