Kambi ya makapera Mwadui yapata pigo Mobby aopoa jiko

Muktasari:

  • Wachezaji wengi wamekua waoga katika kufunga ndoa wakiogopa viwango vyao kufa.

Dar es Salaam. Beki wa Mwadui Fc, Idd Mobby amefunga pingu za maisha na mchumba wake wa muda mrefu Ilham Tungu.

Mobby na Ilham wamedumu kwa muda mrefu katika mahusiano ya uchumba kabla ya baadae kufunga pingu za maisha.

Awali walianza Send Off iliyofanyika Ijumaa na Jumapili walifunga pingu za maisha mkoani Shinyanga.

Beki huyo nahodha wa muda mrefu katika kikosi cha Mwadui, ni miongoni mwa mabeki visiki katika Ligi Kuu Bara.

Mobby ana uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji kama ambavyo mara kwa mara alikuwa akitumiwa na kocha wake Ally Bizimungu.