Kagere agoma mbio za mfungaji bora akifikisha mabao 22 Ligi Kuu

Sunday May 19 2019

 

By Imani Makongoro

Dar es Salaam.Mpachika mabao nyota wa Simba, Meddie Kagere amesema anacheza Ligi si kwa kushindana na mtu.
Kagere ametoa kauli hiyo mara baada ya kufikisha mabao 22 kwenye Ligi Kuu Leo baada ya mchezo kati ya Simba na Ndanda ulioisha kwa Ndanda kufungwa 2-0.
"Najipa chalenji mimi mwenyewe, sipewi chalenji na mtu yoyote ndiyo sababu nafunga," alisema Kagere mara baada ya mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mbali na Kagere, Simba sasa inahitaji ushindi katika mchezo unaofatia ili iweze kutangaza ubingwa msimu huu.

Simba imebakisha michezo mitatu ili kumaliza msimu, huku wakihitaji kutetea ubingwa wao kwa mara nyingine.

Advertisement