KMC pungufu yapania kuiduwaza Simba Kirumba leo

Thursday April 25 2019

 

By Oliver Albert

Dar es Salaam. Pamoja na kuwakosa nyota wake wanne kocha wa KMC, Ettiene Ndayiragije amesema vijana wake wako tayari kupambana na Simba na kupata pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika leo Alhamis jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika mchezo huo KMC itawakosa wachezaji wanne Charles Ilamfia, Emmanuel Mvuyekule, Mohammedy Rashid na Elius maguri.

Pia, KMC itaikabili Simba huku ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata walipokutana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Ndayiragije alisema wachezaji wake wana kiu ya ushindi hivyo wataingia katika mchezo huo wakiwa na lengo moja tu kupata pointi zote tatu.

"Ushindi ndio kitu muhimu kwetu kwani tunazihitaji pointi tatu ambazo zitatuweka nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kwa sababu bado hatuko sehemu salama.

Ndayiragije alisema Simba ni timu kubwa hivyo watu watarajie mpira mzuri huku akiwataka wachezaji wake kupambana na kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili wajiongezee kujiamini.

Advertisement

 

 

Advertisement