JKT Queens’s yaichapa Alliance Girls

Saturday June 9 2018

 

By Saddam Sadick

Mwanza. Alliance Girls imeshindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kuchapwa bao 1-0 na JKT Queens katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake.


Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, ulikuwa wa kwanza kwenye raundi ya pili na wa nane katika Ligi hiyo na JKT kuibuka kifua mbele.


Licha ya timu zote kusakata kandanda safi na kuvutia kwa wadau wa soka waliojitokeza uwanjani hapa, wenyeji walishindwa kufurukuta na kujikuta wakilala kwa kibano hicho.


Bao la dakika ya 63 lililofungwa na Fatuma Swalehe akiunganisha krosi safi ya Asha Rashid lilitosha kuipa pointi tatu timu yake.


Kwa matokeo hayo, JKT wanafikisha pointi 24 na kukaa nafasi ya kwanza, huku Alliance wakibaki nafasi yao ya nne baada ya mechi nane kwa timu hizo.

Advertisement