Ilanfya aililia AS Kigali

Friday August 9 2019

 

By Charity James

MSHAMBULIAJI wa kikosi cha KMC, Charles Ilanfya amesema majeraha aliyoyapata yaliyosababisha ashindwe kucheza mchezo wa awali dhidi ya AS Kigari yamezima mipango yake ya kuipambania timu kuhakikisha inaingia hatua inayofuata.
KMC inatarajia kushuka dimbani kesho kucheza mchezo wa mtoano Ilanfya amesema mipango yake ya kuisaidia timu yake kufanya vyema katika mashindano ya Kombe la Shirikisho imeshindwa kutimia.
Alisema anasumbuliwa na nyama za paja majeraha aliyoyapata akiwa katika maandalizi ya mchezo huo ikiwa ni sambamba na Ligi kuu Tanzania Bara, kuweka wazi kuwa mungu akijaalia anaweza kuungana na timu ikirejea kutoka huko.
"Nilikuwa na mipango ya kuhakikisha napata nafasi ya kufunga katika mchezo huo endapo ningepewa nafasi na mwalimu lengo ni kuamini kuwa bao langu au mabao yangeweza kuivusha timu katika hatua inayofuata," alisema.
"Hakuna mchezaji ambaye amesajiliwa kwaajili ya kuongeza idadi ya namba kikosini kila mmoja anamalengo yake mimi nilitamani pia kutumia mashindano hayo kujitangaza kimataifa naamini timu yangu itapata nafasi ya kuendelea hatua inayofuata nitapata nafasi ya kucheza tena," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Mwadui Shinyanga.

Advertisement