VIDEO: Huzuni yatawala Simba! Mbuzi wawili watumika kisomo cha MO

Friday October 12 2018

 

Dar es Salaam. Viongozi, wanachama na mashabiki wa Simba pamoja na mbuzi wawili wameingia ndani ya ukumbi tayari kwa kusoma dua ya kumuombe Mohammad Dewji 'MO' apatikane akiwa salama.

Mapema leo Uongozi wa Klabu ya Simba ulitangaza uamuzi wa kufanya kisomo saa 8 mchana baada ya sala ya Ijumaa makao makuu ya Simba, Msimbazi kwa ajili ya kumuombea Dewji ‘MO’ aliyetekwa na watu wasiojulikana jana alfajiri.

Tayari mchana huu muitikio umekuwa mkubwa kwa watu kujitokea huku ndani ya ukumbi ni masikitiko na kushangaa kutekwa kwa tajiri huyo.

Huku baadhi ya Wanawake wamesema wamefunga kuhakikisha tajiri huyo anarejea anaungana nao pamoja na familia yake.

"Jamani ni mtu wa watu, Mungu amkumbuke na kumuepusha na maswahiba, yaani mpaka tunashindwa kufanya vitu muhimu."

Angalau kwa upande wa wanaume unaonekana kusikika vicheko, wakati mwingine wanachanganya stori sio kama wanawake wanaoonekana muda wote kuhoji nini kimemkuta ‘Mo’.

Advertisement