Huko Ifakara mashabiki wa Simba, Yanga wakomoana

Saturday May 11 2019

 

By JUMA MTANDA

MOROGORO. Nyie mjue hizi timu za Simba na Yanga zina mashabki wengi aise lakini mashabiki wake kumbe wana vituko huko kitaa unaambiwa.

Sasa huko katika Mji wa Ifakara ambako ndiko makao makuu ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, mashabiki wa klabu hizo wapo kibao.

Katika halmashauri ya wilaya ya Kilombero, kuna watumishi kibao ambao kila mmoja ana mapenzi na timu hizo kongwe na nyingine.

Mmoja wa watumishi katika idara ya ustawi wa jamii halmashauri hiyo ni, Latifa Kalikawe kumbe yeye ni shabiki wa kutupwa wa wekundu wa Msimbazi na humwambii kitu na timu hiyo.

Mwanaspoti ilinasa mazungumza kati ya Latifa Kalikawe na mmoja wa madereva wa halmashauri hiyo mjini Ifakara, Latifa akieleza namna anavyoipenda na kuisapoti Simba Sc katika michezo ya ligi kuu na ile ya kimataifa.

Latifa alieleza Simba ndio timu anayoipenda na amelazimika kununua kingÌamuzi ili kuifuatilia akitoka kazini lakini wageni wanaotembelea kwake na kukuta mchezo wa Simba inachezwa na timu nyingine itakubidi uisapoti Simba na sio timu pinzani ujue.

Advertisement

ÏNimenunua kingÌamuzi kwa ajili ya kuifuatilia Simba inapocheza michezo yake tu na sio timu nyingine kwani mimi ni mshabiki wa Simba sasa inakuwaje niifuatulie timu nyingine ? (Yanga, Azam Fc, Mtibwa Sugar).alihoji Latifa.

Baada ya wageni wanaenda nyumbani kwake kumbe na wenyewe ni mashabiki wa timu nyingine na wanaposhangilia timu zao wanazopenda ni kama wanamkera afisa huyo.

Unaambiwa baada ya hao wanaenda kwake na kukuta mchezo wa mnyama ukionyeshwa kwenye luninga na kuishangilia timu pinzani sasa hivi amewakomesha kwa kutolipia kifurushi cha sport katika kingÌamuzi chake.

Eti kwa sababu nyumbani kwake watu wanaojazana kufuatilia michezo wamekiuka masharti kwa kushangilia timu pinzani na Simba Sc wamekuwa wakimkejeli pindi timu yake ya simba ikifanya vibaya

Timu zilizotembeza kipigo mbele ya Simba ni pamoja na Mbao Fc, Kagera Sugar na michezo ya kimatifa ni TP Mazembe, AS Vita, Al Alhal na nyingine katika ligi ya mabingwa hasa michezo ya ugenini sasa maneno ya kejeli ya mashabiki hao katika michezo hiyo kumbe ilikuwa ikimkasirisha Latifa tena nyumbani kwake.

"Sijalipia kifurushi cha michezo kwa sababu watu wanaokuja nyumbani kwangu kuangalia soka ligi kuu wamekuwa wakiangalia timu pinzani na simba na watu hao anawajua kumbe ni mashabiki wa Yanga." alisema Latifa.

Sasa Latifa anafuatilia timu yake kupitia simu janja kama sehemu ya kuepukana na maneno ya kejeli kutoka kwa mashabiki wa Yanga hasa wale wanaonda nyumbani kwake kuangalia mpira kwa kutonunua kifurushi cha michezo kama njia ya kuwakomoa.

Advertisement