He! Lukaku anataka kwenda Juventus

Muktasari:

Straika, Romelu Lukaku hajafuta uwezekano wa kuihama Man United na kwenda kujiunga na Juventus kwa siku za baadaye baada ya kukiri kwamba anakoshwa na wababe hao wa Serie A.

ROMELU Lukaku ameamua kutikisa kiberiti huko Manchester United. Straika huyo namba moja kwenye kikosi hicho cha Jose Mourinho amesema haoni kwanini asihamie Italia, huku akiitaja Juventus kuwa kuna marafiki zake kibao kwenye kikosi hicho.
Maneno hayo ya Lukaku yameonyesha dhahiri  hana maisha marefu kwenye kikosi hicho cha Old Trafford huku akikiri mipango yake ni kwenda kucheza katika timu ya Mabingwa wa Serie A, Juventus.
Man United itacheza na Juventus kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, na Lukaku alipoulizwa kama anawaza siku moja kwenda kujiunga na Juventus, alisema: "Kwanini isiwe? Naamini hilo litatokea."
Straika huyo amefunga mabao manne tu kwenye Ligi Kuu England msimu huu amechukua nafasi hiyo kumsifu Kocha Massimiliano Allegri na wachezaji wake huko Juventus kabla ya mechi yao.
"Juve ina mipango mizuri imewekwa sawa na wanasonga mbele tu. Kila mwaka wanajaribu kujiimarisha. Bila ya kusitasita, Juventus ni moja kati ya timu mbili au tatu bora za Ulaya. Ina kocha mzuri kwenye benchi na wachezaji mahiri katika kila nafasi. Cristiano Ronaldo yupo sawa na kuna wengine pia wa kuwatazama.
"Paulo Dybala ameonyesha mambo makubwa na yupo vizuri, lakini mimi nampenda sana Douglas Costa. Ni usajili wa aina yake na siku zote ameonyesha anaweza kufanya mambo tofauti ndani ya uwanja."

SUMMARY
Straika, Romelu Lukaku hajafuta uwezekano wa kuihama Man United na kwenda kujiunga na Juventus kwa siku za baadaye baada ya kukiri kwamba anakoshwa na wababe hao wa Serie A.

&&&