He! Aliyefanana na Messi azushiwa

Thursday June 27 2019

 

TEHRAN, IRAN.MTU mmoja aliyefanana na Lionel Messi huko Iran, Reza Parastesh amekanusha tuhuma za kwamba alilala na wanawake 23 tofauti akijidai yeye ni supastaa wa Barcelona.

Kumekuwa na madai huko kwenye mitandao ya kijamii mtu huyo wa Iran amekuwa akitumia kufanana kwake na Messi kuwarubuni wanawake na kulala nao.

Lakini mwenyewe amekanusha tuhuma hizo na kusema hajawahi kutenda kosa kama hilo. Parastesh alisema: “Taarifa hizo zimesambaa kwenye nchi za Kiislamu jambo ambalo ni shida kubwa.

Nimekuwa nikipata matatizo makubwa sana kwa sababu jambo hilo. Familia yangu imekuwa ikinisakama pia kwa jambo hilo.”

Mtu huyo mwenye maskani yake huko Tehran na kujishughulisha na mambo ya mitindo alitoa video yake maalumu kwenye Instagram akikanusha jambo hilo.

Advertisement