Hazard tayari kaaga viongozi Chelsea

Tuesday May 14 2019

 

EDEN Hazard amekamilisha msimu wake wa saba wa Ligi Kuu ya England akiwa mchezaji wa Chelsea na kisha akabainisha kuwa ameifahamisha klabu hiyo kuhusu mpango wake wa kwenda kujiunga na Real Madrid.

”Nimeshafanya maamuzi yangu lakini hayanitegemei mimi pekee,” alisema Hazard baada ya sare ya bila magoli dhidi ya Leicester. “Nimeiambia klabu wiki kadhaa zilizopita.

Chelsea watarejea kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao, pointi moja waliyoipata dhidi ya Leicester ilitosha kuwafanya wamalize katika nafasi ya tatu, lakini Hazard amesema jambo hilo halitabadilisha chochote katika uamuzi aliofanya.

Anasema yuko tayari kusaka changamoto mpya, lakini Real Madrid ni lazima waafiki bei ya kumng’oa kutoka katika mkataba wa mwaka mmoja aliobaki nao.

Advertisement