Hazard bado aiota Chelsea, huku akiri Madrid kiboko

Saturday August 10 2019

 

By Thomas Ng’itu

WINGA mpya wa Real Madrid, Eden Hazard amesema hawezi kusahau maisha aliyoishi akiwa katika kikosi cha Chelsea kwa misimu yote aliyokuwa hapo.

Hazard alisema licha ya kuishi vizuri akiwa na Chelsea, ameweza kukutana na maisha tofauti akiwa na klabu yake mpya ya Real Madrid.

“Tangu nikiwa mtoto nilikuwa naota nitakuja kuvaa jezi ya Madrid, sasa Madrid wakikugongea mlango kitu kilichofuata ni kufungua tu,” alisema.

Aliongeza kuwa mchezaji wa Madrid kumemfanya kutimiza vitu vingi ambavyo alipanga kuvitimiza, lakini pia kufundishwa na kocha ambaye alikuwa anatamani kuwa kama yeye kipindi anacheza.

“Zinedine Zidane ni mmoja ya watu ambao nilikuwa najifunza vingi kutoka kwao kipindi nakuwa, nilikuwa naweka picha zake chumbani kwangu lakini hivi sasa ni kocha wangu.’’

Advertisement