Hazard azidi kuigonga kichwa Real Madrid

Thursday May 16 2019

 

WIKI hii habari kubwa ambayo imetawala ni juu ya nyota wa Chelsea, Eden Hazard kuwa katika hatua nzuri ya Kuhamia Real Madrid kwa ada ya Pauni 86 milioni.

Habari hizo zilikolea utambi baada ya mchezaji huyo kuweka wazi kwamba aliongea na viongozi wa timu yake juu ya nia ya kuondoka katika klabu ya Chelsea wiki mbili zilizopita huku kitu ambacho kilikuwa kikisubiriwa ni suala la Real kuweka fungu mezani.

Hata hivyo habari za ndani zilizopatikana kutoka Chelsea zinasema kuwa dili hilo linasuasua na huenda uamuzi wa kumwachia mchezaji huyo ukawa mgumu kwa kuwa Chelsea inataka fungu la Pauni 100 milioni ili kumwachia mchezaji huyo.

Mtu mmoja kutoka ndani ya Chelsea alisema anafahamu kwamba Real wamekuwa wakimnyemelea mchezaji huyo kwa muda mrefu lakini kama pesa hiyo haitatolewa basi shughuli nzima inaweza kuishia hapo na ndoto za staa huyo zitakuwa zimefikia ukingoni kwa sasa.

Advertisement