Hawa: Baada ya tabu sasa ni wakati wa kucheka

Muktasari:

Hawa amekaa nje ya muziki miaka miwili amerudi tena katika tasnia hiyo baada ya Naseeb Abdul 'Diamond' kusaidia fedha za matibabu.

Dar es Salaam. Mwimbaji wa Hawa Said ametoa sababu za kuachia wimbo mpya unaoitwaa ‘kucheka’ ni kutokana na mambo magumu aliyopita.

Hawa aliyekuwa nje ya muziki huo kwa muda wa miaka miwili kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya moyo alisema alipokuwa anaumwa hakuwahi kufurahi muda wote ilikuwa ni kilio.

Alisema wimbo wake huo ametoa zawadi kwa mashabiki wake ikiwa ni sambamba na Watanzania wote waliokuwa wakimfariji alipokuwa kitandani anaumwa.

"Nimeumwa muda mrefu kitu pekee ambacho nilikuwa nakikumbuka ni kicheko kwani sikumbuki kama kunasiku nilipata furaha muda wote nilikuwa mtu wa huzuni tu kutokana na hari niliyokuwanayo," alisema na kuongeza kuwa.

Anamshukuru Mungu kwa mpa nguvu ya kupambana tena na kufanikisha suala la kuachia kazi hiyo ambayo anabainisha kuwa imemshindisha njaa lengo lake lilikuwa ni kuona anaikamilisha.

"Sina Meneja na sikuwa na msaada hadi nimeikamilusha kazi hiyo mtu pekee ninaeweza kumshukuru ni mama yangu kwani ndiye aliyekuwa anasimamia suala la chakula tangu naanza kuandaa video hadi inakamilika," alisema.

Hawa alisema mama yake kaandaa chakula cha watu nane ambao wamehusika katika utayarishaji wa video hiyo kuanzia mwanzo hadi wanamaliza.