Hasheem Thabeet sasa kuiongoza Tanzania kikapu

Muktasari:

Kwa upande wa timu ya taifa ya wanawake chini ya Kocha, Agnela Semwaiko itaundwa na wachezaji Winfrida Zabron, Orline Londo, Jesca Ngisaise, Hadija Kalambo, Noela Mwenda, Fatma Yasoda, Lulu Joseph, Juliana Mwita, Martha Mashaka na Liliana Solidon.

NYOTA wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet ni miongoni mwa wachezaji 34 waliochaguliwa kuunda Timu ya Taifa ya Tanzania itakayoshiriki mashindano ya Kanda ya Tano ya Afrika yanayotarajiwa kuanza Juni 25 hadi Julai Mosi mwaka huu, kule Uganda.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF), Pahers Magesa alisema wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Magesa alitaja kikosi hicho kitakachoongozwa na Kocha Ashraf Haroun kuwa ni Thabeet(USA), Haji Mbegu, Jackson Brown, Moses Jackson, Gwalugano John, Gilbert Batungi, George Tarimo na Cornelus Petar.

Wengine ni Erick John, Ally Mohamed, Baraka Sadiki, Enerico Agustino, Alinan Adrew, Yahaya Malim (Zanzibar), Murshid Mudrikat (USA), Mwalimu Heri, Amin Mkosa, Fadhiri Chuma, Swedi Mayala,Sudi Ulanga,Tyrope Edward na Qurash Sylvester (Uganda). Nyota wengine ni Yassir Kassim, Alpha Kisusi (Canada), Jimmy Brown (Phillipino), Mussa Chacha, Solomoni Anelos, Omar Malim (Uganda) na Abdalah Ramadhani ‘Dulla’ (Shelisheli).

Kwa upande wa timu ya taifa ya wanawake chini ya Kocha, Agnela Semwaiko itaundwa na wachezaji Winfrida Zabron, Orline Londo, Jesca Ngisaise, Hadija Kalambo, Noela Mwenda, Fatma Yasoda, Lulu Joseph, Juliana Mwita, Martha Mashaka na Liliana Solidon.

Wengine ni Doritha Mbunda, Faraja Malaki, Neema Kibonde, Tukusubira David, Maoureen Sizya (Uganda), Diana Katembo, Dawa Haji, Irene Mollel na Habiba Mustafa (Uganda).