Hapatoshi Kombe la FA, Simba, KMC, Azam vitani

Muktasari:

Keshokutwa Jumamosi kipute hicho kitaendelea kwa michezo nane kupigwa viwanja tofauti huku Simba ikiikaribisha Mwadui FC kwenye Uwanja wa Uhuru huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa bao 1-0 kwenye Ligi Kuu mchezo uliofanyika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga lililofungwa na Mathias Mdamu.

Dar es Salaam.Vumbi la Kombe Shirikisho la Azam lianza kutimka kesho Ijumaa na mwishoni mwa wiki kwa miamba Simba, Yanga na mabingwa watetezi Azam kushuka kwenye viwanja mbalimbali kusaka nafasi ya kusonga hatua ya 16 bora.

Kesho Ijumaa KMC watakuwa wenyej wa Pan Africans kwenye Uwanja wa Uhuru, wakati Panama FC kutoka Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) itavaana na Mtwivila ya Ligi Daraja la Pili (SDL).

Keshokutwa Jumamosi kipute hicho kitaendelea kwa michezo nane kupigwa viwanja tofauti huku Simba ikiikaribisha Mwadui FC kwenye Uwanja wa Uhuru huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa bao 1-0 kwenye Ligi Kuu mchezo uliofanyika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga lililofungwa na Mathias Mdamu.

Nayo Gwambina FC atakipiga na Ruvu Shooting, African Sports itaikaribisha Mkwakwani Alliance FC, Ihefu FC itavaana na Gipco wakati Ndanda FC ikikipiga na Dodoma FC.

Michezo mingine bingwa wa kombe la Mapinduzi,  Mtibwa Sugar atakipiga na Sahare All Stars, JKT Tanzania itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo kucheza na Tukuyu Stars wakati Kagera itakuwa Kaitaba kuivaa Kitayosa FC.