Haaland kuwa mbadala wa Mbappe Real Madrid

REAL Madrid inaweza kuhamia kwa straika wa Borussia Dortmund, Erling Haaland ikiwa itashindwa kuinasa saini ya Kylian Mbappe kutoka PSG ambayo imekuwa ikiitamani tangu msimu uliopita.

Hata hivyo ilishindwa baada ya uchumi kuyumba kutokana na janga la corona.

Madrid imekuwa ikihaha kujenga safu ya ushambuliaji ambayo imepwaya tangu kuondoka kwa Cristiano Ronaldo huku Karim Benzema umri wake ukionekana kupepea.

Haaland anaangaliwa kama mbadala wa Mbappe ambaye ndio chaguo la kwanza, lakini kuna uwezekano PSG isiwe tayari kumuachia na ikiwa itamuuza itamuuza kwa pesa ndefu.

Mkataba wa Haaland unatarajiwa kumalizika mwaka 2024 na bei yake huenda ikawa rahisi ukilinganisha na ile ya Mbappe ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2022.