Gwambina yaibukia uwanja wa nyumbani

GWAMBINA wakiwa katika Uwanja wao wa nyumbani (Gwambina Complex), wamepata ushindi wa mabao 2-0, katika mechi ya mzunguko wa sita Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar kutokea Manungu Morogoro.

Mabao hayo mawili ya Gwambina yalifungwa na Yusuph Dunia dakika ya 20, kwa mkwaju wa penalti baada ya makosa yaliyofanywa na beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Job kushika mpira ndani ya boksi mwamuzi kuamuru kuwa ni penalti na kumuonyesha kadi ya njano.

Dunia amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao la penalti kwa msimu huu tangu uanze.

Bao la pili lilifungwa dakika 87, na Meshack aliyepiga shuti kali na ushindi huo umekuwa faida kwa Gwambina kuongeza pointi tatu ambao kwa mara ya kwanza wanacheza katika Uwanja wao wa nyumbani tangu ulivyo fungiwa kutokana na kutokuwa na hali nzuri kwenye eneo la kuchezea.

Baada ya kupata ushindi huo Gwambina wameongeza pointi tatu ambazo zimewafanya kufikisha pointi saba na kupanda mpaka nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi.

Mtibwa Sugar baada ya kipigo hiko watabaki na pointi zao tano na kutoka nafasi ya 11, waliokuwepo na kushuka nafasi ya 13.

Baada ya mechi hiyo kumalizika saa 1:00 usiku kutakuwa na mechi nyingine ya muendelezo wa ligi kati ya wenyeji Azam Fc, ambao watakuwa katika Uwanja wa Azam Complex, kucheza dhidi ya Mwadui.