Gumbo akumbukwa Bunju

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba , marehemu Omary Gumbo mwenye shati jekundu

Muktasari:

Gumbo alikumbwa na mauti katikati ya mwezi uliopita na kuzikwa jijini Dar es Salaam na jana Dalali alipopata nafasi ya kuzungumza alianza kwa kusema;

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba , marehemu Omary  Gumbo amekumbukwa katika maonyesho ya uwanja wa klabu hiyo uliopo Bunju B nje kidogo ya jiji la Dar es Salam.
Gumbo aliongoza kipindi hicho wakati Simba ipo chinibya Hassan Dalali aliyekuwa Mwenyekiti na Mwina Kaduguda akiwa Katibu Mkuu.
Dalali alimkumbuka Gumbo mara baada ya kukabidhiwa kipaza sauti na Msemaji wa Simba, Haji Manara akimpa heshima kiongozi huyo wa zamani ambaye alitafuta eneo la kujenga uwanja wao.
Gumbo alikumbwa na mauti katikati ya mwezi uliopita na kuzikwa jijini Dar es Salaam na jana Dalali alipopata nafasi ya kuzungumza alianza kwa kusema;
"Kwanza kabisa tumkumbuke marehemu Gumbo ambaye nilikuwa naye wakati wa uongozi wangu tukiwa na akina Kaduguda, hivyo ni mmoja wa watu muhimu katika mafanikio ya Simba.
"Lakini kwenye mafanikio hayo tusiache kumbuka Mareheno Chano. Pia nampongeza Mohamed Dewji kwa jitihada hizi za ujenzi wa uwanja, alisema anatoa pesa yake mfuko lakini hata sisi tulifanyakazi Simba kwa kujitolea hivyo Simba kila mmoja ajitolee kulta mafanikio ya klabu," alisema Dalali
Dalali amewataka wanasimba wote kujitoa uwanjani kuisapoti timu yao na hata kunapokuwa na matatizo wajitokeze kushirikiana.
Awali, Manara alisema uwanja wao leo Jumamosi ni maalumu kwa ajili ya kuwaonyesha wanachama wao hatua waliyofikia na kuanza kuutumia kwa ajili ya mazoezi lakini Januari mwakani ndio utazinduliwa rasmi.
Katika shughuli hii imehudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingisa, Dalali, Kaimu Mwenyekiti Mwina Kaduguda, Asha Baraka, Selemani Haroub, Huseein Kita ambao ni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na baadhi wachezaji wa zamani Malota Soma, Hamza Maneno na  Abdallah Kibadeni.