Guardiola kumtuliza Kompany huko Etihad

Muktasari:

Pep anafahamu ugumu wa kupata beki wa aina ya Kompany na anaamini kama ikishindikana basi atamshawishi nyota huyo wa Ubelgiji arudi.

MANCHESTER,England.BEKI wa Manchester City, Vincent Kompany ameweka wazi anaondoka katika klabu hiyo kwenda Anderlecht ambako anatarajiwa kuwa kocha mchezaji, lakini kocha wake, Pep Guardiola naye kaibuka na yake.

Pep anasema mchezaji huyo ataondoka kama alivyopanga, lakini atamrudisha haraka iwezekanavyo. Kompany amekuwa na Man City kwa miaka 11 na amepata mafanikio makubwa huku kombe ambalo amelikosa likiwa ni la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Jumamosi iliyopita alipata Kombe la FA na hilo lilikuwa kombe la tatu msimu huu mengine yakiwa ya Ligi Kuu England na Kombe la EDL.

Kwa sasa ana miaka 33 anaona ni wakati mwafaka wa kurudi kwao Ubelgiji katika klabu yake ambayo alianzia kucheza soka la kulipwa na amefurahia kuwa kocha mchezaji.

Pep anafahamu ugumu wa kupata beki wa aina ya Kompany na anaamini kama ikishindikana basi atamshawishi nyota huyo wa Ubelgiji arudi.

“Ni mtu ambaye nimemzoea, nafahamu nitamkumbuka sana. Lakini namhakikishia atarudi tu katika klabu hii. Ni ngumu kusema kwaheri, alikuwa nahodha makini sana,” alisema Pep.