Fulham ndio basi Ligi Kuu England

Muktasari:

  • Kocha wa muda, Scott Parker alishindwa kuikoa Fulham na janga la kuteremka daraja tangu alipotwaa mikoba ya aliyekuwa mtangulizi wake, Claudio Ranieri.

LONDON, ENGLAND.FULHAM imeteremka daraja licha ya kubaki na michezo mitano mkononi, baada ya kuchezea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Watford katika mechi ya Ligi Kuu England.

Klabu hiyo imeteremka daraja baada ya kuwekeza kiasi cha Pauni 100 milioni katika usajili wa wachezaji 12 majira ya kiangazi msimu uliopita.

Baada ya mchezo kumalizika, wachezaji wa Fulham walionyesha kusikitishwa na matokeo hayo kwenye Uwanja wa Vicarage Road.

Kocha wa muda, Scott Parker alishindwa kuikoa Fulham na janga la kuteremka daraja tangu alipotwaa mikoba ya aliyekuwa mtangulizi wake, Claudio Ranieri.

Watford imeonyesha kiwango bora msimu huu na haikushangaza kupata ushindi huo ulioipa pointi tatu.

Wakati Fulham ikiteremka daraja, Manchester United ilipata matokeo mabaya kwa kufungwa mabao 2-1 na Watford juzi usiku.

Man United ilikosa nafasi ya kukwea hadi nafasi ya tatu kutokana na kipigo hicho ambacho hakikutarajiwa na wengi.

Timu hiyo ilicheza pungufu baada ya nahodha wake, Ashley Young kulimwa kadi nyekundu dakika ya 57 baada ya kupewa kadi mbili za njano.

Pengo la beki huyo mkongwe wa kulia, lilionekana baada ya Wolves kucheza kwa kiwango bora na kupata mabao hayo mawili.

Man United ipo nafasi ya tano katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 61 sawa na Tottenham Hotspurs, lakini ina uwiano mzuri wa idadi ya mabao.

Liverpool inaongoza ikiwa na pointi 79 ikifuatiwana Manchester City (77) na Arsenal ipo nafasi ya tatu kwa pointi 63.