Ferguson tabasamu kama lote, Man United yaua

Muktasari:

  • Tangu Ferguson ameondoka Old Trafford, Man United haijawahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England

London, England. Tabasamu limerejea kwa Sir Alex Ferguson baada ya Manchester United kurudi katika wimbi la ushindi ukiwamo ushindi wa jana usiku wa Kombe la FA wa mabao 2-0 dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja Stamford Bridge

Mabao ya Ander Herrera na Paul Pogba yalitosha kuivusha Man United kucheza kwa robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Wolves kwenye Uwanja wa Molineux hapo Machi 16.

Ni ushindi mwingine kwa kijana wa Ferguson, Ole Gunnar Solskjaer, ambaye alicheza kwa misimu 11 akiwa chini ya yake kama mchezaji kati ya mwaka 1996 na 2007.

Tangu alipoondoka Jose Mourinho Desemba mwaka jana, Ferguson mwenye miaka 77, amekuwa akionekana mara kwa mara katika mazoezi ya timu hiyo pamoja na mechi.

Ferguson alifanya upasuaji wa ubongo Mei 5 mwaka jana, alionekana kwa mara ya kwanza akitazama timu hiyo Septemba 22, 2018.

Hata hivyo jana alionekana mwenye afya njema  na furaha baada ya timu yake kushinda magharibi mwa London.

Ushindi huo wa Solskjaer umerudisha timu yake katika mstari wa ushindi baada ya kufungwa mechi ya kwanza na Paris Saint-Germain katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora.