Familia ya Messi yamchenjia Maradona

Muktasari:

Maradona amesema Messi hafai kuwa kiongozi kwenye timu kwa sababu amekuwa na kawaida ya kwenda chooni mara 20 kabla ya mechi

FAMILIA ya Lionel Messi imemjia juu Diego Maradona baada ya kutoa maneno ya kashfa kwa staa huyo wa Barcelona na Argentina.
Maradona, alimshambulia Messi kwa maneno makali kuwa anapoichezea Barcelona anakuwa tofauti kabisa na anapokuwa kwenye kikosi cha Argentina huku akidai hana vigezo vya kuwa nahodha kwa sababu amekuwa na kawaida ya kwenda chooni mara 20 kabla ya mechi.
Maneno hayo yameikera familia ya Messi na kuamua kumjibu Maradona, ambapo binamu wa staa huyo wa Nou Camp, Maxi Biancucchi alisema Maradona ambaye kwa sasa anapaswa kukaa kimya na kukabiliana na tatizo la kunenepeana na uteja ni mpuuzi mkubwa.