Eti pesa za urithi? Siri ipo hapa nyie

Friday January 11 2019

 

By Rhobi Chacha

MITOKO ya bata batani inayofanywa na staa wa Bongo Movie, Irene Uwoya imekuwa ikiwaumiza watu vichwa na huko kwenye mitandao ndio kama moto umewashwa unaambiwa kwani, watu hawatulii.

Yaani kila kukicha Uwoya katupia picha ama video akiwa viwanja akiponda raha huku pamba na mwonekano wake ukizidi kuwavuruga watu akili huku wengine wakihoji siri ya kupenda kwake.

Lakini, hilo la bata limekuwa likenda sambamba na vichambo vya nguvu ambapo, Uwoya wamekuwa wakirushiana na mumewe Dogo Janja, ambaye kwa sasa mambo sio shwari hata kidogo na kila mmoja ameshika hamsini zake.

Kila mmoja anasema lake, ambapo baadhi wanadai kuwa Uwoya amebamba kibosile mwenye pesa zake, wapo wanaodai kuwa ni urithi wa mumewe wa awali, marehemu Hamadi Ndikumana ambaye wamezaa mtoto mmoja.

Lakini, wengine wakaenda mbali zaidi kwa kudai kuwa msanii huyo kwa sasa anaenjoy mafao ya kustaafu kwa mzazi wake. Hata hivyo, mambo yoote hayo kwa Uwoya amesema kamwe hayana ishu kabisa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Uwoya amesema ameamua kuchagua maisha anayopenda hivyo anashangazwa na watu kumfuatilia wakitaka kufahamu anapata wapi pesa za kujirusha.

“Watu bwana! Ningekuwa niko rafu wangesema, ninapendeza bado wanasema pia, jamani nimeamua kuchagua maisha yangu. Kupendeza hapa ndio nyumbani kwake na sijaanza leo kabisa, japo sina fedha lakini kidogo nilichonacho kinaficha umasikini. Sasa watu wanaponiona niko tofauti na kuanza kuzusha la kuzusha sioni kama ni sawa,” alisema Uwoya na kuongeza: “Watu wakumbuke kuwa nafanya biashara na matangazo nje ya nchi, na hivyo vitu ndio vinanipa jeuri na sio hayo mambo wanayodai.

“Niwape pole kwa wanaosubiri kuona maisha yangu ya sasa yanabadilika, nashangaa kuna watu wanasema mambo bila uhakika, wanadai pesa za urithi wa Ndikumana, mara mzazi wangu kastaafu mara sijui natoka na nani… mnapata tabu bure tu.”

Kuhusu ishu ya vijembe kwenye mitandao ya kijamii na Dogo Janja, Uwoya hakutaka kuweka wazi akisema kwamba, huwa hamlengi mtu bali anaposti tu kama ilivyo vitu vingine.

“Sidhani kama ninachoweka katika ukurasa wangu wa Instagram huwa namlenga mtu, inatokea tu mtu unajiandikia maneno basi mwingine akahisi anasemwa yeye, lakini sirushiani vijembe na mtu,” alisema Uwoya ambaye kwa sasa amekuwa mkali anapoulizwa jambo

Advertisement