El Ghazi: Nimeamini mpira ndio maisha yangu

Tuesday March 24 2020

El Ghazi, Nimeamini mpira ndio maisha,Kiungo wa Aston Villa, Anwar El Ghazi,virusi vya ugonjwa wa Corona,

 

By Thomas Ng'itu

Kiungo wa Aston Villa, Anwar El Ghazi amesema kukaa nje kwa muda wa takribani wiki mbili tayari ameshamisi kuuchezea mpira.

Ligi nyingi zimesimama kujilinda na virusi vya ugonjwa wa Corona ambavyo vinasambaa kwa kasi katika nchi mbalimbali duniani.

"Mazoezi nayo yalisimamishwa nadhani tutaanza wiki hii Jumatano kwa kufanya kwa makundi, muda huu nipo zangu tu nyumbani," alisema.

El Ghazi alisema anajihisi upweke mkubwa kwa kipindi hiki na ameshagundua kwamba hatoweza kuishi bila kuuchezea mpira.

"Inaonyesha kabisa kwamba mpira ndio maisha yangu, unajua nilishazoea kabisa kuamka na kwenda mazoezini kujiandaa kwa mchezo ujao, lakini sasa hivi nakimbia kidogo, nafanya mazoezi madogo kwangu lakini sijihisi kama nimefanya kitu kwa siku," alisema El Ghazi.

Advertisement