EPL wikiendi hii usipime

Muktasari:

Machester City pia watakua ugenini kucheza na Norwich City ambao wamepoteza michezo mitatu na kushinda mchezo mmoja kati ya minne ya ligi iliyopita huku Manchester city wakishinda mitatu na kutoa sare mchezo mmoja.

BAADA ya mapumziko mafupi kupisha mechi za timu za Taifa, wikendi hii Ligi Kuu England inarudi ambapo kesho Jumamosi Septemba 14,  mechi saba zitapigwa viwanja tofauti.
Katika mechi hizo watu wengi wanasubiri kuona vigogo wa soka nchini humo kama Liverpool, Manchester United, Chelsea na Manchester City watafanya nini.
Liverpool ambao tangu ligi imeanza hawajapoteza mchezo wowote watakuwa uwanja wa nyumbani kuwakaribisha Newcastle United ambao mechi nne zilizopita wameshida moja, kutoa sare moja na kufungwa mbili.
Manchester United wao watakua nyumbani 'Old Traford' kuwakribisha Leicester City, mechi hii itakua kali kutokana na mwenendo wa Manchester United kutotabirika huku wenzao Leicester  wakiwa kwenye kiwango bora maana mechi nne zilizopita wameshinda mbili na kutoa sare mbili, huku wenyeji Manchester United wameshinda mechi moja, sare mbili na kufungwa moja na Crystal palace.
Chelsea chini ya kocha wao Frank Lampard watakua wakikipiga ugenini dhidi ya Wolverhampton Wanderers 'Wolves' ambapo mechi nne za ligi ku zilizopita 'The Blues' wameshinda mchezo mmoja, sare mbili na kupoteza mmoja huku wapinzani wao Wolves wakitoa sare mechi tatu na kufungwa moja dhidi ya Everton.
Machester City pia watakua ugenini kucheza na Norwich City ambao wamepoteza michezo mitatu na kushinda mchezo mmoja kati ya minne ya ligi iliyopita huku Manchester city wakishinda mitatu na kutoa sare mchezo mmoja.
Tottenham Hotspur watakuwa nyumbani kuwakaribisha Crystal Palace ambao mechi za ligi nne zilizopita wameshinda mechi mbili, sare moja na kupoteza moja wakati wenyeji Tottenham wakishinda moja sare mbili na kupoteza moja.
Mechi nyingine za ligi hiyo kesho zitakua kati ya Brighton and Hove Albion dhidi ya Burnley huku Sheffield United watakua nyumbani kuwakaribisha Southampton.