Dunia inawasubiri wababe Fury Vs Wilder

Thursday February 13 2020

Dunia inawasubiri wababe Fury Vs Wilder,mabondia wawili Tyson Fury , Deontay Wilder ,Ligi ya Kikapu Marekani ,NBA,

 

DESEMBA 27, siku ambayo ilianza kusisimua wapenzi wa mchezo wa ngumi, ndandi ama ndonga pale ambapo mabondia wawili Tyson Fury na Deontay Wilder walipofumua mwanzo wa uwepo wa pigano lao la marudiano baada ya kupita mwaka na ushee walipomalizana kibabe.

Hii ni baada ya Desemba 2018 kutoka suluhu wakimaliza kwa droo ya 113-113 katika pambano lililokuwa kali lililopigwa katika Ukumbi wa Staples Center ambao ndio unaotumiwa pia na timu za Los Angeles Lakers na Clippers kwenye mechi zao za nyumbani katika Ligi ya Kikapu Marekani (NBA).

Sasa baada ya kupita mwaka na ushee, hatimaye mabondia hao wanatarajiwa kupigana tena katika pigano la pili wikiendi ijayo Februari 22, ambalo ndilo linatajwa kuamua nani mbabe kati yao na kukata ngembe za pande zote mbili.

Mabondia wote kabla ya kukutana walicheza mapigano tofauti ambapo Tyson Fury alimtandika Mswidishi Otto Wallin, Septemba mwaka jana, wakati ambao Deontay Wilder alitetea mkanda wake wa WBC dhidi ya Luiz Ortiz Novemba mwaka jana, na pambano lao linaendelea kusubiriwa kwa hamu likizidisha msisimko wa kupata mbabe baina yao.

Advertisement