Duh!Aubameyang ampa maujanja Kocha Emery

Muktasari:

  • Arsenal jana Jumapili ilikuwa na kibarua kizito cha kuwakabili mahasimu wao kwenye Ligi Kuu England, Tottenham Hotspur huko Emirates ikiwa ni mechi ya kwanza kuwakutanisha maswahiba Emery na Mauricio Pochettino kwenye soka la England.

LONDON, ENGLAND.STRAIKA, Pierre-Emerick Aubameyang amemwambia Kocha Unai Emery, anahisi anakuwa moto ndani ya uwanja na kucheza soka la kiwango chake kama atapangwa kucheza kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati.

Staa huyo wa kimataifa wa Gabon, Aubameyang mara kwa mara amekuwa akipangwa kwa kubadilishana na Alexandre Lacazette, huku kama mmoja akicheza kati, basi mwingine anacheza pembeni ikitokea Emery ameamua kuwaanzisha kwa pamoja.

Lakini, Aubameyang anajaribu kumwambia kocha wake atapenda zaidi kama atakuwa anachezeshwa kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati na mahali hapo ndipo panapomfaa kuonyesha makali yake mchezoni.

“Napendelea zaidi kucheza kama mshambuliaji wa kati,” alisema Aubameyang.

“Lakini mimi ni mchezaji wa timu. Kama nitahitajika kuwa kwenye wingi, basi nitacheza kwenye nafasi hiyo. Lakini, ninachopendelea ni kucheza straika.”

Arsenal jana Jumapili ilikuwa na kibarua kizito cha kuwakabili mahasimu wao kwenye Ligi Kuu England, Tottenham Hotspur huko Emirates ikiwa ni mechi ya kwanza kuwakutanisha maswahiba Emery na Mauricio Pochettino kwenye soka la England.