Domayo, Peter waanza matibabu Afrika Kusini

Friday October 12 2018

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Wachezaji wa Azam FC kiungo, Frank Domayo ‘Chumvi’ na mshambuliaji, Paul Peter, walianza matibabu jana Alhamisi nchini Afrika Kusini.

Wachezaji hao ambao waliondoka nchini na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ siku ya Ijumaa tayari kwa matibabu hayo.

Domayo ambaye pia anaichezea Taifa Stars na Peter akiichezea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 'Ngorongoro Heroes'.

Wote wana maumivu ya goti waliyoumia hivi karibuni jambo lililowafanya matajiri wao wa Azam kufanya matibabu ya haraka.

Azam ilishafanya hivyo kwa wachezaji wengine kama, Joseph Kimwaga, Domayo na Pascal Wawa ambaye kwa sasa anakipiga klabu ya Simba.

Advertisement