Dodoma yanasa mwingine Ligi Kuu

Muktasari:

Dodoma Fc iliwasajili, Khamis Mcha (Ruvu Shooting), Aboubakary Ngalema (Mbao Fc) na hivi sasa Joseph Mapembe akitokea Biashara Utd.

KLABU ya Dodoma Fc inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza inaendelea kufanya usajili wa  baada ya kusajili nyota wa Ligi Kuu mfululizo kwa ajili ya msimu ujao.
Dodoma Fc imewasajili Khamis Mcha (Ruvu Shooting), Aboubakary Ngalema (Mbao Fc) na sasa Joseph Mapembe kutoka Biashara Utd.
Klabu hiyo pia iliamua kufumua benchi la ufundi baada ya kuachana na kocha Jamhuri Kihwelu ‘Julio’  na sasa ipo chini ya Mbwana Makata.
Sababu kubwa ya Julio kuondolewa inatajwa ni kutotimiza malengo ya kuipandisha timu hiyo Ligi Kuu kama ilivyokuwa kwenye makubaliano yao ya kimkataba.
Kwa upande wa wachezaji hao wote walikuwa wachezaji wa vikosi vya kwanza katika klabu zao msimu uliopita wa Ligi Kuu, hivyo huenda ikawa hesabu nzuri kwa Dodoma FC kutimiza malengo ya kupanda ligi kuu.