Dirisha la usajili England kufunguliwa leo, timu vigogo England kusaka makinda

Thursday May 16 2019

 

London, England. Wakati dirisha la usajili likifunguliwa leo, miamba ya soka England imeingia vitania kuwania saini za wachezaji chipukizi zikitaka kuwasajili katika majira ya kiangazi.

Miamba sita ya Ligi Kuu England Manchester City, Liverpool, Chelsea, Arsenal, Tottenham Hotspurs na Manchester United.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, idadi kubwa ya wachezaji chipukizi wameonekana kutia fora katika usajili wa majira ya kiangazi

Chelsea, Tottenham, Arsenal na United zinaoneana kukamia kusajili wachezaji wenye viwango bora kuziba mashimo ya msimu uliopita.

Timu hizo iliziacha Man City ikitwaa ubingwa na Liverool ikishika nafasi ya pili kwenye ligi hiyo msimu uliopita.

Dirisha la usajili England limefunguliwa leo na litafungwa Agosti 8, mwaka huu, lakini dirisha la usajili wa nje utakamilika baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kufungua Juni 9.

Advertisement

Man City inamtaka kinda wa Benfica Joao Felix mwenye thamani ya Pauni 60 milioni. Arsenal inamtolea macho Ryan Fraser wa Bournemouth na David Neres anayecheza Ajax Amsterdam.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amechuana na klabu nyingine Ulaya kuwania saini ya mshambuliaji kinda wa Ajax Amsterdam David Neres.

Chelsea ipo katika mkakati wa kutaka huduma ya mchezaji kinda Luka Jovic. Kinda wa Fulham Ryan Sessegnon anahusishwa na mpango wa kutua Tottenham majira ya kiangazi.

 

 

Advertisement