Cristiano Ronaldo alianzisha Juventus

Muktasari:

Picha zilisawekwa mtandaoni zilionyesha Mayweather akiwa kwenye picha na Christiano,Ronaldo, Paulo Dybala, Giorgio Chiellini na Blaise Matuidi.

Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo ameanza safari yake ya soka kwa mafanikio nchini Italia baada ya kutwaa taji la kwanza  la Super Cup tangu ajiunge na klabu hiyo msimu.

Junvetus iliifunga AC Milan jana, huku bao la ushindi likiwekwa wavuni na Ronaldo na kuwafanya kunyakua taji la Super Cup.

Tukio la kufurahisha katika mchezo huo ni bondia Floyd Mayweather Jr aliyeungana na wachezaji wa Juventus kwenye chumba cha kubadilishia nguo huku akipiga icha na wachezaji hao.

Picha zilisawekwa mtandaoni zilionyesha Mayweather akiwa kwenye picha na Christiano,Ronaldo, Paulo Dybala, Giorgio Chiellini na Blaise Matuidi.

Ronaldo amefikisha bao la 16 msimu huu tangu alipotua Italia.

Juventus ambao wapo mbele ya Napoli waliopo nafasi ya pili kwa pointi tisa kwenye msimamo wa Serie A watakuwa na kibarua mbele ya Chievo Jumatatu wiki ijayo.